Sunday, 24 April 2016

Mpendwa

Akipita, akipunga
Upepo kamwona Bahari
Samawati, alipendeza
Naye Bahari ‘kampenda Upepo kwa uzuri alioleta
Furaha ilimjaa na kumsukuma upwani
Sabalkheri. Naomba ukae nami, Mpendwa

Uwe Malkia wangu

Ilhali Upepo alikuwa mwenye mwendo mara yote
Upepo alimzunguka Bahari, akambusu, akanena:
Meli yaelea juu yako,
dau yatabaradi  juu yako
Hio hali yao, wewe husongi!
Nikiondoka, samaki wataendapi? Bahari akauliza kwa mshangao mkuu!
Naye Upepo akamjibu: Nikitua, ulimwengu utasongaje?
Laazizi, ulinipendea mie uzuri wangu,
ndio mimi huyu, hamna namna ingine… 


No comments:

Post a Comment